Wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne 2022 wametakiwa kuutumia muda uliobaki kujiandaa kikamilifu kwaajili ya mitihani inayotarajia kuanza hivi karibuni.Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga leo tarehe 20,Oktoba 2022 katika mahafali ya 13 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bupamwa.
“ kati yenu sioni mtu atakaye shindwa mtihani, jitahidini msome kwa bidii tumieni muda uliobaki kujiandaa vizuri matarajio yangu nikuona wote mnaendelea kidato cha tano, wengine waende chuoni wote muendelee na masomo asiwepo wa kuishia kidato cha nne” amesema Msanga
Akisoma risala Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Helman Daudi Shingisha amesema Shule inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wanafunzi wengi kuacha masomo kutokana na umbali mrefu kutoka kwenye makazi yao hadi shule iliko, wengine kulazimishwa kuolewa na kuchunga mifugo. Vilevile amesema Shule inakabiliwa na changamoto ya ukosefu tangi la kuhifadhia maji ili kuepukana na ukosefu wa maji pindi yanapokatika.
Akihutubia watu walioshiriki mahafali hiyo Bi. Happiness amewataka wanafunzi kuyatumia madarasa yanayoendelea kujengwa na Serikali kupata mafanikio katika elimu, vilevile ameahidi kununua tangi la kuhifadhia maji ili kuondoa changamoto ya maji, vilevile amewataka wazazi kupenda elimu ili wawahamasishe watoto wao kupenda shule na hivyo kuzuia changamoto ya ndoa za utotoni na kukabiliana na tatizo la wanafunzi wengi kuacha masomo yao.
Wanafunzi 61 wanatarajia kuhitimu kidato cha nne huku wanafunzi 90 wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo alizozielezea Mkuu wa Shule hiyo.Aidha wanafunzi wa Shule hiyo wameahidi kufanya vizuri katika mitihani inayotarajia kufanyika hivi karibuni.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.