Kata ya Kikubiji ni miongoni mwa kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba zilizopata fedha kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya. Jumla ya shilingi milioni 500 zimeshapokelewa kwaajili ya ujenzi wa Kituo hicho, ambapo awamu ya kwanza ilipokelewa milioni 250 ambazo zimetumika kujenga majengo matatu yaani jengo la wagonjwa wa nje. ( OPD), Maabara na kichomea taka.
Fedha zilizopokelewa awamu ya pili ni milion 250 ambapo majengo matatu yanatarajiwa kujengwa jengo la wazazi,jengo la upasuaji na jengo la kufulia.
Kutokana na mapokezi ya fedha hizo za awamu ya pili wananchi wakishirikiana na watumishi wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi.Happiness Msanga wamechimba msingi wa majengo hayo matatu huku wakiishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta fedha za miradi katika kata hiyo.
“ tunaishukuru Serikali kwa kutuletea fedha za kujenga hiki kituo cha Afya, kata hii tulikuwa hatuna kituo cha Afya kitu kilichokuwa kinapelekea wagonjwa wetu kupelekwa kata ya Bupamwa Kituo cha Mwamashimba kwahiyo kujenga kituo hapa kwetu tumefurahi sana na tunaishukuru Serikali” amesema Mali ya Tabu Kasanga
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya Afya vinne, ambapo vitatu vimepokea fedhaza ujenzi huo katika awamu ya sita ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani na kituo kimoja kimepokea fedha za ukamilishaji.
Aidha Halmashauri inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo huduma za wagonjwa wa nje yaani OPD zinaendelea kutolewa huku ukamilishaji wa majengo mengine yakiwemo majengo ya wodi, jengo la huduma za dharura na jengo la upasuaji yakiwa hatua za mwisho za ukamilishaji.
Sekta hiyo ya Afya imeendelea kuboreshwa, jumla ya zahanati nne zimepokea fedha za ukamilishaji milioni 200, huku Halmashauri kwa kutumia mapato ya ndani ikiendelea kukamilisha zahanati mbili kwa milioni 100
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.