Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka Wananchi wa Kata ya Nyambiti kuishi kwa upendo, kuacha gari la wagonjwa la Kata hiyo liwahudumie wagonjwa wa vituo vya Afya vyote.
Ameyasema hayo leo Oktoba 5,2023 wakati akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata hiyo baada ya Wananchi hao kutaka gari hilo likae kwenye kituo chao tu
" niwaombe muishi kwa upendo gari hilo liacheni lihudumie na vituo vingine kwasababu Kuna vituo vya Afya vingi havina gari nyie mkihitaji gari toeni taarifa gari litakuja kuchukua mgojwa lakini siyo kutaka gari likae kwenu tu wengine wakose huduma" Ludigija
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ametatua changamoto za migogoro ya Ardhi, kero za walengwa wa kaya masikini TASAF, upatikanaji wa maji na umeme.
Naye Mheshimiwa Peter Misalaba Diwani wa Kata ya Nyambiti amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutatua changamoto za Kata hiyo na amemuomba aendelea na utaratibu huo kwani utasaidia kupunguza kero za wananchi.
Baada ya kutatua kero za Wananchi wa Nyambiti Mheshimiwa Ludigija amefika Kata ya Maligisu ambapo ametatua kero za wananchi wa Kata hiyo ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kukata bima ya Afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya na kuepuka kutumia fedha nyingi pindi wanapopatwa na ugonjwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.