Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi shupavu wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendele kuineemesha Kwimba kwa kuleta fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo.
Wananchi wa Kijiji cha Kiliwi Kata ya Bupamwa nao hawajakaa kimya wameishukuru Serikali kwa kuleta fedha milioni 584 kwaajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari itakayojengwa katika Kijiji hicho.
Wameyasema hayo leo Agosti 12,2023 wakati wakichimba msingi wa majengo ya Shule hiyo ambapo madarasa nane,jengo la utawala, maabara tatu, jengo la TEHAMA, jengo la Maktaba ,kichomea tana, tangi la maji na matundu ya vyoo yanajengwa
" tunaishukuru sana Serikali kwa kuleta fedha za Shule watoto wetu walikuwa wanateseka sana kutembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 20 kwenda Sekondari ya Bupamwa Sasa watasoma karibu" amesema Paulo Nyanda
Akiongea na Wananchi hao Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka kuwa walinzi wa mradi huo na kuendelea kutoa ushirikiano pale wanapohitajika kujitoa nguvu kazi
" niwapongeze kwa kujitoa kuchimba msingi na muendelee kujitoa pale inapohitajika nguvu kazi kurahisisha utekelezaji wa mradi huu, pia niwatake muwe walinzi wa mradi huu sitarajii kusikia kuna kifaa kimeibiwa au kupotea" DC Ludigija
Akiwasilisha taarifa fupi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri imepokea Bilioni 1.62 kwaajili ya ujenzi wa Shule mbili za Sekondari ya Bumyengeja Kata ya Sumve na Kiliwi Kata ya Bupamwa na mabweni mawili ambayo moja linajengwa Ngudu Sekondari na jingine linajengwa Sumve na ujenzi wa nyumba za watumishi 2/1 mbili ambapo moja inajengwa katika Shule ya Sekondari Kilyaboya na nyingine katika Shule ya Sekondari Manawa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.