Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupitia shirika la Amref health Africa kwa kushirikiana na AIRish AID wameweza kutoa elimu kwa wananchi wa Wilaya hii juu ya Afya ya uzazi ambapo wanawake wajawazito wameshauriwa kuchukua tahadhari juu ya dalili mbaya zinazoweza kujitokeza kwao kwa mfano mtoto kutocheza tumboni,miguu kuvimba,kutokwa damu,kutokwa majimaji machafu sehemu zao za siri,maumivu makali ya tumbo na dalili nyingine wawahi kituo cha afya kwaajili ya kupata ushauri wa wataalamu na matibabu.
Aidha wananchi wameshauliwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Vilevile wananchi wameshauliwa kujiunga na bima ya Afya iCHF iliyoboreshwa ambayo ni shilingi elfu thelathini (30,000) kwa familia ya watu sita ili waepukane na usumbufu wa kutafuta pesa za matibabu pindi wanapougua au kuuguliwa. Bima hii inamuwezesha mwananchi kutibiwa Hospitali zote za serikali za ndani ya Wilaya na Hospitali ya Mkoa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.