Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewashauri Wananchi wa Wilaya ya Kwimba kupenda maendeleo.Ameyasema hayo leo Oktoba 24,2023 katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Ngudu
" Wananchi pendeni maendeleo, jengeni nyumba nzuri za kupangisha huko icheja Ili mji ukue, wafanyabiashara wekezeni hapa Kwimba jengeni Hoteli, tupambane kuibadirisha Kwimba, nyie mmeona Mheshimiwa Rais analeta fedha nyingi za miradi ya maendeleo na sisi tumuunge mkono kwa kufanya yale yanayowezekana kuibadirisha Kwimba" Ludigija
Katika mkutano huo kero mbalimbali zimewasilishwa na wananchi, Kisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amezitolea majibu na ufafanuzi, ikiwa ni pamoja na umiliki wa vibanda vya stendi ya zamani, uboreshaji wa miundombinu ya soko la zamani, upatikanaji wa ajira katika miradi inayotekelezwa na Halmashauri na mambo mengine.
Naye meneja wa TARURA Mhandisi Kayungi ameutumia mkutano huo kuwashauri wafugaji na wakulima kuzingatia sheria zinazozuia kupitisha mifugo Barabarani na kuacha shughuli za kilimo kwenye hifadhi za barabara kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria na hatua kari zitachukuliwa kwa wote wanaokiuka sheria hiyo.
Katika mkutano huo ameshiriki Katibu mwenezi CCM Wilaya ya Kwimba Ndugu Shija Malando ambaye amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kusikiliza kero na kuzitatua pia amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
" nimpongeze Mkurugenzi anasimamia miradi ya maendeleo vizuri, hospital imekamilika, kantini,kliniki ya mifugo, vituo vya Afya na miradi mingine inakamilika kwa wakati endelea hivyo na sisi CCM tutaendelea kuwasimamia ili mtekeleze Ilani kama inavyotakiwa"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.