Kijiji cha Shigangama Kilichopo Kata ya Shilembo ni miongoni mwa vijiji ambavyo havina visima Wala mabomba ya maji, Wananchi wa Kijiji hicho wametoa kero hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija leo Oktoba 10,2023 wakati akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata hiyo
" tunateseka sana kupata maji tunatembea zaidi ya kilomita tisa kwenda kutafuta maji, tunamuomba Rais atusaidie tupate visima au maji ya ziwa Ili tuepukane na adha hii" amesema Mwalu Joseph
Kupitia kero hiyo Mkuu wa Wilaya amewataka RUWASA kutatua kero hiyo kwa kuangalia upatikanaji wa maji kwa kuyavuta kutoka maeneo jirani au kuchimba visima katika Kijiji hicho
" Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuleta fedha za miradi ya maji Ili kumtua mama ndoo kichwani sasa niwatake RUWASA muangalie uwezekano wa kufikisha maji hapa" Ludigija
Aidha Mkuu wa Wilaya amefika Kata ya Ilula ambapo amekutana na changamoto ya maji kukatika zaidi ya wiki mbili hapo ametatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza wasimamizi wa maji kutengeneza mashine iliyokuwa imeharibika na ameondoka eneo hilo baada ya maji kupatikana.
Katika ziara hiyo Mheshimiwa Ludigija ametatua kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na migogoro ya ardhi, upatikanaji wa umeme na amewahamasisha wananchi kuanzisha miradi ya maendeleo kama ujenzi wa Zahanati, nyumba za Walimu na miradi mingine
" mnahitaji Zahanati lakini bado hamjaanzisha hata boma niwashauri muanzishe jengo kama vijiji vingine wanavyofanya ili muweze kuwekwa kwenye bajeti ya ukamilishaji" Ludigija
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.