Wananchi waadhimisha siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo tarehe 26,Aprili 2022 kwa kushiriki uchimbaji wa msingi wa madarasa matatu na matundu sita ya Choo.
Akiongea na Wananchi baada ya kushiriki uchimbaji wa msingi, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amesema anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Kiongozi Shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za miradi katika Wilaya ya Kwimba.
" Shule hii ya kabale ilikua na miundombinu chakavu sana hadi madarasa mengine ilibidi yabomolewe ili kuepusha majanga yanayoweza kutokea, sasa tumejenga madarasa sita kwa fedha za mapato ya ndani ambapo miliono 121 zimetolewa na Halmashauri, lakini leo tunachimba msingi wa madarasa matatu na msingi wa Choo matundu sita baada ya kupokea milion 80 kutoka Mfuko wa kunusuru Kaya masikini TASAF" amesema Samizi
Kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi waliokuwa wakisoma katika mazingira magumu na yasiyorafiki kwa ujifunzaji kupata Elimu katika mazingira sahihi, hii itachochea ari ya ujifunzaji.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo Bi. Happiness Msanga amesema Halmashauri imetoa fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa sita katika shule ya Kabale, pia wanayo mikakati ya kukarabati Shule zenye miundombinu chakavu, na kuongeza madawati katika shule zenye uhaba wa madawati, viti na meza.
Kukamilika kwa madarasa hayo kunatarajiwa kuwa chachu kwa Wanafunzi kupenda Shule na masomo kitu kitakachosaidia kupunguza changamotto ya utoro na hivyo kuongeza ufauru kwa wanafunzi wa Shule hiyo.
Walimu nao hakuachwa Halmashauri inatarajia kujenga ofisi ya Walimu baada ya ukamilishaji wa madarasa sita ambayo yako hatua za ukamilishaji.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.