" Nasisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji haijalishi vinatumika sasa, vilitumika zaman au vitatumika badae" haya ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Samizi wakati wa kikao cha Mwaka cha tathimini ya huduma za maji vijijini kilichofanyika leo tarehe 18,Mei 2022 katika ukumbi wa Pam.
Katika kikao hicho Wananchi wametakiwa kutunza vyanzo vya maji vinavyotumika na visivyotumika ili kuwe na uhakika wa upatikani wa maji kwa wakati wote.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wasimamizi wa maji ngazi ya jamii kuhakikisha wanatoa Elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kutumia maji ya bomba na visima vinavyojengwa kwa lengo la kuwarahisishia upatikanaji wa maji.
Mkuu huyo amevitaka vyombo vya wasimamia maji ngazi ya jamii kuwa na msimamo dhabiti katika kutoa huduma ya maji na kuhakikisha kila chanzo cha maji wanchokisimamia kinaendelea kujiendesha bila kuhitaji usaidizi, katika hilo amewataka kuweka bei za maji ambazo hazitawaumiza Wananchi lakini hazitafanya chanzo kishindwe kufanyiwa ukarabati pale unapohitajika.
Katika kikao hicho wadau wa huduma za maji wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta miradi mikubwa ya maji katika Wilaya ya Kwimba.
"sisi tunamshukuru sana Rais kwa kutuletea mradi mkubwa wa maji wa bilion 8.4 katika Kata ya Hungumalwa kwani mradi huu ukikamilika hatutakuwa na tatizo la maji tena" amesema Majid Idrisa Mbelwa mwenyekiti Kamati ya Watumia maji LUHUNYAKI
Wilaya ya Kwimba inayo malengo ya kutoa maji kwa asilimia 85 kwa mwaka huu wa fedha ambapo mpaka kufikia leo RUWASA imefikia asilimia 72 ya kuwafikishia maji Wananchi vijijini.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.