Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Joachim Msanga awaomba Wananchi wa Kata ya Bungulwa kuwa Walinzi na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Bungulwa. Ameyasema haya leo tarehe 18, Oktoba 2021 katika kijiji cha Isunga ambapo uchimbaji wa msingi kwaajili ya ujenzi wa Kituo hicho umeanza leo.
Akiongea na Wananchi wa Kata hiyo amewataka wanawake wote kuwa tayari kushiriki kutowaachia wanaume kwani Kituo hicho kikikamilika kitawapunguzia shida ya kwenda umbali mrefu kutafuta huduma za Afya.
" sisi wanawake ndio tunaojifungua mara kwa mara tupo hospitali,sisi ndio tunaouguza waume zetu na watoto wetu wakilazwa kwaio tuone umuhimu wa kushiriki katika usimamizi na ujenzi wa kituo hiki ili tuondokane na adha ya kwenda mbali kutafuta huduma za Afya". amesema Happiness Msanga
Katika Shughuli hiyo Kamati ya Ulinzi na usalama wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Nyakia Ally wameshirikiana na Wananchi wa Kata ya Bungulwa katika zoezi la uchimbaji wa msingi wa Kituo hicho.
Katibu Tawala amewataka Wananchi kushiriki katika ujenzi wa kituo hicho ili kiweze kukamilika kwa wakati na huduma za kiafya zianze kutolewa, amesisitiza kuwa Wananchi wote wanapaswa kuwa tayari kushiriki ujenzi, kulinda vifaa vya ujenzi na kuwa tayari kutoa taarifa pindi watakapoona wizi wa aina yoyote ile bila kujali mwizi ni nani.
Zoezi hilo la uchimbaji wa msingi limeshirikisha viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) ambao wameweza kuongea na Wananchi na wakawataka wananchi wote kuwa tayari kusimamia ujenzi huo ili Ilani ya Chama iweze kutekelezwa kama Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan alivyokusudia.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.