Wananchi wa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza wameshiriki sherehe za Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 08/03/2017 ikiwa na kauli mbiu “ Tanzania ya viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi”
Madhimisho yameanzia viwanja vya Halmashauri kupitia viunga mbalimbali vya mji wa Ngudu hadi viwanja vya mpira wa miguu KWIDECO na kupokelewa na mgeni rasmi ndugu Andrea Ng’wani kwa niaba ya mkuu wa wilaya.
"Mnaombwa kukemea na kuacha vitendo vya kuwazuia watoto wa kike wasipate elimu ili kuwaozesha. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano imeweka mpango wa makusudi kabisa katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya msingi na kuendelea hasa mtoto wa kike, na ina kaulimbiu inayosema Elimu bure, hivyo kila mtoto apelekwe shule kwa wakati na asikatizwe masomo yake kwa sababu zisizokuwa na msingi, ikiwemo kuwaozesha katika umri mdogo na kuwafanya walezi wa familia. Serikali ipo makini katika kuzuia mdondoko wa watoto wa kike shuleni na kupambana na mimba za utotoni”
Hayo yamesemwa na Ndg Andrea Ng`wani katibu Tawala wa Wilaya kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya kwimba wakati akiwahutubia wananchi na amesisitiza kwa kusema
Mzazi yeyote au Jamii itakayohusika kwa namna yoyote ile kumkatiza mtoto wa kike masomo Sheria itachukua mkondo wake.
Wakati wa akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Bibi Getrude Nokingile amesema Wanawake wengi hasa wazee na vikongwe waishio vijiji wanaishi pekee yao na wanaishi katika mazingira hatarishi,ambayo yanawafanya waonekane tofauti na watu wengine na baadhi ya watu kuhisi kwamba kutokana na hali duni ya maisha wanayoishi ni wachawi, ndio wanaosababisha vifo vya watu katika maeneo wanayoishi.Tunaomba serikali kuanzia ngazi ya kitongoji hadi ngazi ya Wilaya kushirikiana na wananchi katika kuwatambua na kuwalinda ili waishi kwa usalama na amani.
Mwanamke ni mlezi wa familia, ni msingi wa maendeleo na ni kiongozi shupavu wa famililia hayo yamesemwa na Ndugu Innocent Sililo mkazi wa mtaa wa chamhela wilayani kwimba wakati wa sherehe hizo.
Aidha Bibi Sobi Masalu mamaye ni mkuu wa Kitengo cha Sayansi kimu Idara ya Elimu Msingi amesisitiza kuwa ili mwanamke aweze kukidhi kauli mbiu ya mwaka huu anahitaji Elimu ya ujasiliamali, Mtaji, mfumo dume kuondolewa, stadi za ujuzi mbalimbali na hasa za maendeleo zifundishwe kwa msisitizo kuanzia madarasa ya chini na somo la S/Kimu lirudishwe shule za msingi ili mtoto anapomaliza elimu ya msingi awe na maarifa ya kumwezesha kupambana na mazingira yanayomzunguka.
Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa kuwapa vyeti walimu wa kike kumi katika shule za Msingi na Sekondari wilayani humo ambao wamefaulisha vizuri mitihani ya Taifa 2016/2017.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.