Wananchi washiriki uzinduzi wa uchimbaji wa msingi wa madarasa 14 kwaajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi katika kijiji cha Kadashi leo tarehe 1 Agosti, 2022.
Akiongoza uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amesema Wilaya ya Kwimba inaupungufu wa madarasa zaidi ya elf moja kwa Shule zà Msingi hivyo inahitajika nguvu na mali ili kufanikisha ujenzi huo.
Mhe. Samizi amewataka Wananchi kuwa tayari kujitolea nguvu na mali ili kufanikisha ujenzu huo
" haya madarasa tunayaanzisha sisi wananchi hatuna fedha ililetwa kutoka Serikalini hivyo niwaombe kila mtu kwa nafasi yake awe tayari kuchangia kuanzia tofari moja na kuendelea ili tuweze kufanikisha ujenzi wa boma kwanza"
Kutokana na hamasa iliyofanyika wananchi wamejitolea kununua mchanga, mawe na wengine matofari ili kuanzisha ujenzi huo. Mbunge wa Jimbo la Sumve naye amejitolea mawe na matofari 2000.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameitumia nafasi hiyo kutoa elimu ya sensa kwa Wananchi, amewataka kuachana na imani potofu kuhusu sensa, " lengo la sensa nikupata takwimu sahihi ili Serikali iwezo kutoa huduma kulingana na idadi ya watu, hivyo niwaombe muwe tayari kuhesabiwa wote hata walemavu msiwafiche siku hiyo watoeni wahesabiwe" amesema Samizi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.