Akiongea katika Hafla ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 1 Disemba ambapo kiwilaya yamefanyika katika Kata ya Bupamwa, Kijiji cha Mhalo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwinba Ndugu Ally Nyakia amewataka wananchi wote kutafakari mienendo yao kama inawapelekea kupata maambukuzi ya UKIMWI au kuwakinga na ugonjwa huo.
"Kila mtu atafakari mwenendo wake kimaisha kuona kama mwenendo huo unamuweka katika mazingira hatarishi yakupata virusi vya UKIMWI au yanamkinga na virusi" amesema Nyakia
Amesisitiza kuwa maadhimisho ya siku ya UKIMWI yanafanyika kwa lengo la kukumbushana kila mtu amefanya nini katika kuhakikisha maambukizi yanadhibitiwa. Amewataka Wananchi kujilinda na kuwalinda watoto wao hasa vijana ambao bado wanasoma ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao kwani watu wengi wakishapata Upungufu wa Kinga Mwilini(UKIMWI) malengo yao huvurugika na kisha kukosa mwelekeo na hivyo kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Katibu Tawala huyo amesisitiza kuwa Wilaya ya Kwimba inaendelea kuboresha huduma za Afya ili kuwasaidia watu wanaoishi na virus vya UKIMWI kupata huduma za kiafya katika maeneo wanayoishi bila kutembea umbali mrefu kufata huduma za Afya.
Aidha Serikali inaendelea kutoa fedha kwaajili ya kuboresha huduma za Afya ambapo kwa sasa Wilaya ya Kwimba inaendelea na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,Vituo vya Afya vitatu yaani Kadashi,Bungulwa na Kikubiji ambavyo vikikamilika vitaongeza upatikanaji wa huduma za Afya katika maeneo hayo na kuwapunguzia wagonjwa adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.