Wananchi wa Kijiji cha Maligisu washauriwa kupanda miti ili kutunza mazingira yanayowazunguka kwa faida ya sasa na badae. Ameyasema Mheshimiwa Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Kwimba leo tarehe 23 Feb,2022 katika Uzinduzi wa kampeni ya kutunza mazingira kwa kupanda miti na kusafisha mazingira.
Katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi kujenga tabia ya kupenda usafi ikiwa ni pamoja na kujenga Choo bora inayosafishika
" niwatake Wananchi wote mpande miti katika maeneo yenu hasa miti ya matunda ambayo hamtaweza kuikata hovyo vilevile hakikisheni kila familia inakuwa na choo kizuri kinachosafishika choo hiyo itumike siyo mnajenga choo ya kuonyesha kwa viongozi halafu hamuitumii"
Mkuu huyo amesisitiza kuwa utunzaji wa mazingira utasaidia kupata mvua itakayowezesha kilimo kuendelea hivyo chakula kitapatikana kwa wingi.
Aidha Mheshimiwa Samizi amefika Kata ya Wala na kuwataka wafanyabiashara na Wananchi wa Kata hiyo kutotumia mitaro ya kupitishia maji kama sehemu ya kutupa taka. Amesisitiza utunzaji wa mazingira ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kujitokeza kutokana na uchafu wa mazingira.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.