Wanawake wawili wa Kijiji cha Malemve kitongoji cha Mwang'alanga wameuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali usiku wa kuamkia leo tarehe 29 Aprili,2022.Akiongea kwa maskitiko Mwenyekiti wa kijiji hicho amesema waliofariki ni Mama na Binti yake waliojulikana kwa majina ya Shikalile Masala miaka 75 na Mariam Deogratias miaka 36.
Kwa mujibu wa maelezo ya Watoto walioshuhudia tukio hilo wanasema watu walimavia nyumba hiyo wakamuua mama yao kwanza kisha wakamuua Bibi yao.
Kutokana na tukio hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mhe.Johari Samizi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amefika mahali hapo akiwa na Kamati ya Usalama na kuongea na Wananchi wa kijiji hicho.
Mhe.Samizi amekea kitendo hicho na amelitaka jeshi la police na Sungusungu kushirikiana ili kuwabaini wauaji.
" hiki ni kitendo cha ukatiri uliopitiliza jamani roho haina mbadara,tuwe na hofu ya Mungu hivi hizi Dini zinawasaidia nini? huyu Bibi alikosea nini hadi auwawe hivi, huyu Mama ameacha watoto wataishije? Sungusungu hakikisheni mnashirikiana na Police kuwapata walifanya tukio hili" amesema Samizi
Aidha Mkuu huyo amewataka Waganga wa kienyeji wanaofanya ramli chonganishi kuacha mara moja tabia hiyo maana maeneo mengi mauaji yanasabishwa na imani za kishirikina. Pia amewataka Sungusungu kuimarisha ulinzi, na Wananchi kutoa taarifa pindi wanapowaona watu wasiowafahamu katika maeneo yao na kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahalifu wote waliopo kijijini hapo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.