Vikundi 39 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vilivyopatiwa mikopo isiyo na riba inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri vimepatiwa mafunzo ya kuendeleza miradi yao, elimu ya umuhimu wa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Haya yamejitokeza leo tarehe 03 /02/2022 katika hafla ya kurasimisha mikopo iliyotolewa kwa wajasiliamari wa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.
Akiongea na wajasiliamari hao Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amewashauri wajasiliamari kuanzisha miradi mbalimbali itakayowawezesha kuzalisha fedha hizo ili wanaporejesha mikopo waweze kubaki na mitaji ya kuendeleza biashara zao.
Aidha Mkuu huyo amesema mikopo yote inayotolewa inapaswa kurejeshwa kwa wakati ili watu wengine waweze kupata mikopo hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imeendelea kutoa Mikopo isiyo na riba kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.Akitoa taarifa ya fedha zilizotolewa Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Rozalia Magoti amesema jumla ya milioni 187,033,483.17 imetolewa kwa vikundi 39 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa pindindi cha mwaka 2020/2021.
Mikopo yote inayotolewa na Halmashauri inapaswa kurejeshwa ndani ya mwaka mmoja hivyo wajasiliamari wote wanaopata nafasi ya kupata mikopo hiyo wanapaswa kuirejesha kwa wakati ili wanufaika wengine waweze kukopeshwa fedha hizo.
Mikopo hiyo imekuwa mkombozi kwa vikundi hivyo kwani vijana wengi wameweza kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa samani za nyumbani, majeneza, ushonaji, ufugaji , uuzaji wa nafaka na shughuli nyingine zinazowawezesha kupata kipato.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.