Kaya 7841 za wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF zanufaika na mpango huo, akiongea na walengwa hao Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi S.Ngaga ambaye amefanya ufuatiliaji kuona zoezi la ugawaji wa fedha hizo linavyofanyika amewashauri walengwa wa TASAF kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.Mhe. Ngaga amesema wanafunzi wanunuliwe mahitaji yao ya Shule kama mpango unavyoelekeza,watoto wanaopaswa kupelekwa kliniki wapelekwe,ujasiliamali mdogomdogo kama ufugaji wa kuku,mbuzi na vitu vingine ufanyike ili familia hizo ziweze kujikwamua kutoka kwenye hali ya umaskini.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewashauri walengwa wa TASAF kujiunga na BIMA ya Afya iCHF iliyoboreshwa ili wawe na uhakika wa matibabu pindi wanapopatwa na magonjwa.Walengwa wa TASAF wanaishukuru Serikali kwa mpango huo wa kunusuru kaya masikuni kwani kupitia mpango huo wengi wao wameweza kujenga nyumba na kupaua kwa bati hali hii imewafanya kupiga hatua kutoka nyumba za nyasi hadi za bati.
Malipo kwa ajili ya mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili dirisha la malipo ya Novemba -Disemba,2020 yamefanyika kuanzia tarehe 13-20/02/2021 katika vijiji vyote vilivyomo kwenye mpango wa TASAF.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.