Halmashauri ya wilaya ya Kwimba,katika kutimiza azma yake ya kupunguza umaskini kwa kutumia wataamu wake imeamua kuendesha mafunzo na kuwapatia mikopo vikundi vya vijana na wanawake kutoka kwenye mfuko wa wanawake na vijana (WDF&YDF).Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Ndg Pendo Malabeja wakati akifungua mafunzo hayo.Aidha aliendelea kusisitiza kwa kusema "Umaskini utatolewa na sisi wenyewe kwenye kaya zetu na siyo mtu mwingine kutoka nje”
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa tukirudisha riba na mikopo kwa muda muhafaka siku moja tutakuwa na Bank ya wilaya ya kwimba ya vikundi vya wanawake na vijana.Pamoja na hayo aliviahidi vikundi hivyo vya ushirika kuvitembelea katika maeneo yao ya kazi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.