Watendaji wametakiwa kutumia pikipiki Kwa kazi zilizokusudiwa ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa miradi na kazi nyingine. Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi.Happiness Msanga Leo Februari 22,2023 wakati akikabidhi pikipiki tisa Kwa Watendaji wa Kata zilizo pembezoni na zinazoongoza Kwa ukusanyaji wa mapato.
" hamjapewa pikipiki kwenda kufanya biashara ya boda boda, katumieni usafiri huu kurahisisha kazi zenu za kukusanya mapato, kusimamia utekelezaji wa miradi na kazi nyingine zote za Serikali" amesema Msanga
Aidha watendaji hao wametakiwa kutunza vyombo hivyo Ili vitumike Kwa muda mrefu na Kwa malengo yaliyokusudiwa, wamesisitizwa kutumia Kwa uangalifu kwani vyombo hivyo ni mali ya Serikali hivyo atakayeharibu au kupoteza atachukuliwa hatua Kwa mujibu wa Sheria.
Watendaji hao wamesisitizwa kuongeza juhudi katika kusimamia mashamba darasa yanayotarajiwa kuanzishwa kwenye Kata zao kwani hawatakuwa na kisingizio cha kushindwa kufika mashambani kwa kigezo cha umbali.
Nao watendaji wameishukuru Serikali Kwa kuona umuhimu wa kuwapatia usafiri utakaorahisisha utendakazi wao "tunaishukuru Serikali Kwa kutupatia pikipiki ambazo zitaturahisishia kazi zetu hasa ukusanyaji wa mapato maana wengine vijiji tunavyosimamia viko mbalimbali sana kwahiyo bila usafiri inakuwa ngumu kufika maeneo yote Kwa wakati, kwahiyo kupitia hizi pikipiki kazi zetu zitaboreshwa zaidi" amesema Salum.M Salum Mtendaji Kata ya Hungumalwa
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.