Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wanasimamia Kila kijiji kuadhimisha wiki ya lishe ya Kijiji ili wananchi waweze kupata Elimu ya lishe bora na kuhakikisha wanatokomeza utapiamlo
" Watendaji hakikisheni hakuna Kijiji kinachoacha kuadhimisha wiki ya lishe Ili hiyo wiki itumike kutoa Elimu ya lishe bora, simamieni Elimu itolewe ili tuepukane na utapiamlo na udumavu" Ludigija
Watendaji hao wametakiwa kuhamasisha unyonyeshaji salama ambao unamtaka mtoto kunyonya miezi sita ya mwanzo bila kupewa chakula hii inasaidia watoto kuepukana na udumavu.
Aidha Mheshimiwa Ludigija amewataka Watendaji hao kusimia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ya kazi ikiwemo miradi inayotekelezwa na TASAF, TARURA na RUWASA
" simamieni miradi tunataka kuona Mtendaji unajua Kila hatua ya mradi unaotekelezwa kwenye eneo lako, miradi yote iliyokwenye Kata yako"
Naye Mratibu wa Lishe Emma Kalolo akiwasilisha taarifa ya lishe ya robo ya kwanza ya mwaka 2023/24 amesema Halmashauri inaendelea kutoa matibabu kwa watoto wanye utapiamlo,pia Elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu lishe bora Kwa wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano na unyonyeshaji salama.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.