Afisa tawala ( W) Ndug. Ally Nyakia akiongea na watendaji wa kata kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amewaelekeza watendaji wa kata kusimamia na kupunguza hali duni ya lishe kwa watoto ili kuondoa tatizo la watoto wenye utapiamlo.
Akielezea majukumu ya watendaji wa kata katika kuhakikisha suala la lishe kwa watoto linaboreshwa Afisa lishe(W) Dr.Emma Kalolo amesema watendaji wanawajibu wa kuhakikisha lishe ni ajenda ya kudumu ili waweze kulifatilia kila wakati,kuibua na kuchochea fursa za lishe katika kata zao,kuhakikisha mpango kazi wa lishe unajumuisha chakula na lishe,usafi wa mazingira ,maji na uchangamshi kwa watoto wadogo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji(W) Ndug. Stahimili Ndaro amewashauri watendaji kulichukulia Jambo hili la lishe kwa uzito ili kuondokana na watoto wenye utapiamlo katika Wilaya ya Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.