Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imekabidhi mashine za kukatia risiti za ushuru (POS)84 kwa watendaji huku wakisisitizwa kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za ukusanyaji wamapato,
“ nawaelekeza kwenda kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifi, kateni ushuru kwa uaminifu zingatieni sheria za ukusanyaji wa mapato, POS zikafanye kazi iliyokusudiwa natarajia kuona mapato ya robo mwaka ijayo yaongezeke zaidi” amesema Mkurugenzi wa Halmashauri Happiness Msanga
Bi. Happiness Msanga amesema Kwa miezi mitatu iliyopita Halmashauri imekusanya zaidi ya asilimia 30 ya bajeti ya mwaka mzima hivyo kutokana na ongezeko la mashine 84 zaukusanyaji mapato wanatarajia kukusanya zaidi ya asilimia 50 ya makusanyo yanayotarajiwa kwa robo ya pili ya mwaka.
Watendaji waliokabidhiwa vifaa hivyo wameahidi kwenda kufanya kazi kwa umakini na uadilifu, vilevile wamesema mashine hizo zitasaidia ukusanyaji wa mapato ukilinganisha na hapo awali ambapo mashine zilikuwa chache hivyo kuyafikia maeneo yote ilikuwa ni vigumu kitu kilichokuwa kinasababisha utoroshaji wa mazao.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amewataka Watendaji wote kufanya kazi zao kwa umakini na uadilifu,pia amewasisitiza Watendaji wote kuhakikisha wanasimamia miradi ya mendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao. Vilevile amewataka watendaji kuitumia mikutano na mikusanyiko mbalimbali inayojitokeza katika vijiji vyao kukemea Imani potofu( zakishirikina ) zinazosababisha kutokea mauaji ya watu, wengi wao wakiwa ni wanawake na wazee.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.