Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Joachim Msanga amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kurudi kwenye msitari ili kufanya kazi kulingana na taratibu, kanuni, sheria na miongozo ya utumishi. Ameyasema haya kwenye kikao kilicholenga Mkurugenzi huyo kujitambulisha kwa Watendaji na kukumbushana taratibu na miongozo ya kazi, kilichofanyika tarehe 09,Sept 2021 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu.
Bi. Happiness amewapongeza Watendaji wote wanaotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu, sheria na kanuni za utumishi wa Umma kisha akawaasa wale wanaofanya kazi kwa mazoea kuacha haraka tabia hiyo.
Aidha amewasisitiza uwajibikaji, kushirikiana, upendo, uadilifu na usimamizi mzuri wa miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ya kazi pia amewataka kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa uaminifu na kujiepusha na ubadhilifu wa aina yoyote ile
"acheni kufanya kazi kwa mazoea, sitakubali ubadhilifu nikakuchekea nitawachukulia hatua wale wote watakaotaka kwenda kinyume na utaratibu" amesema Bi.Happiness
Kikao hicho kimehudhuliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mhe. Theleza Lusangija ambapo amewashauri watendaji kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ya kazi ili inapokamilika iendane na thamani ya fedha zilizotumika pia amewashauri kufanyakazi kwa upendo na ushirikiano.
Katika kikao hicho Watendaji wa Kata na Vijiji wameomba kupewa motisha pale wanapofanya kazi vizuri, hasa wanapotimiza malengo waliyojiwekea katika mpango kazi wao wa kila mwaka.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.