Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amewataka watendaji wa Kata kuwahamasisha wananchi kujenga vyoo bora.
Ameyasema hayo leo Julai 12,2024 wakati wa kikao cha tathmini ya lishe cha robo mwaka " kafanyeni ufatiliaji na muwe wakali familia ambazo hazijajenga vyoo zichukulieni hatua, hakikisheni kila familia inakuwa na choo bora ili tuepuke magonjwa"
Mheshimiwa Ludigija amewasisitiza watendaji kuwatumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutoa elimu ya uzazi wa mpango na unyonyeshaji salama ili kuwakinga watoto na utapiamlo
" toeni elimu kwa wananchi, pia watumieni wahudumu wa afya ngazi ya jamii kufikisha elimu ya afya, unyonyeshaji na uzazi wa mpango"
Aidha amewataka watendaji kushirikisha jamii katika mambo ya maendeleo kama kushiriki ujenzi wa vyoo vya shule na miradi mingine.
Akiwasilisha taarifa ya lishe ya robo mwaka mratibu wa Lishe Emma Kalolo amesema elimu ya lishe bora inaendelea kutolewa kwa wananchi hali iliyopelekea idadi ya watoto wagonjwa wa utapiamlo kupungua kutoka wagonjwa 228 hadi wagonjwa 176 kwa mwaka
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewasisitiza watendaji kuitumia siku ya lishe ya kijiji kuwaelimisha wananchi umuhimu wa lishe bora na madhara ya utapiamlo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.