Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Dkt. Amon Mkoga amekabidhi Pikipiki tatu kwa Watendaji wa Kata za Iseni,Mwandu na Mwankulwe.Pikipiki hizo zimetolewa leo Septemba 5,2024.
Akikabidhi vyombo hivyo vya usafiri Mkoga amewataka watendaji kwenda kuzitumia vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi.
Aidha Mkoga amewataka watendaji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma " fanyeni kazi kwa uadilifu, ukikusanya fedha za mapato peleka Benki usikae na fedha ya Serikali nyumbani"
Akiongea na watendaji hao wa Kata Mkurugenzi amewasisitiza kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula shuleni " wahamasisheni wazazi wachangie vyakula ili wanafunzi wote wapate chakula siyo wengine wanakula wengine wamewaangalia" amesema Mkoga
Naye Afisa Utumishi ( W) Bi. Jane Malongo amewataka watendaji waliokabidhiwa pikipiki kwenda kuzitumia kwa uangalifu, pia amesema jumla ya watendaji wa kata 15 wanavyombo vya usafiri na watendaji 15 waliobaki wataendelea kununuliwa taratibu kadri fedha zitakavyopatikana" hairuhusiwi kuuza mali ya Serikali bila kibali cha mwajiri kwahiyo kila mnachofanya zingatieni kanuni"
Watendaji waliopewa Pikipiki wameshukuru kwa kupata vyombo hivyo vya usafiri na wameahidi kuvitumia vizuri kuongeza ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.