Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kwimba Ndg Stamili Ndaro amewataka watoa huduma ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya kushiririki mafunzo ya mifumo ya Kielektronikia kwa umakini wa hali juu ili waweze kusimamia uzalishaji na uhifadhi sahihi wa taarifa na takwimu za afya pamoja na taarifa sahihi za matumizi ya fedha.
Ndg Ndaro ameyasema hayo wakati wa akifungua mafunzo ya siku sita yaliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wawakirishi kutoka PS3 makao makuu Dar es salaam, PS3 Mkoa wa Mwanza, TAMISEMI na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto katika ukumbi wa Chama Cha Walimu (CWT) Ngudu tarehe 19 Machi, 2018.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kielektronikia ngazi ya kutolea huduma wakifanya mazoezi kwa vitendo baada ya maelekezo kutoka kwa wawezeshaji.
Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Mradi PS3 Mkoa wa Mwanza Ndg Perestian Masai amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo ili kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma kupitia fedha za ruzuku vinakuwa na mfumo maalum wa kuandaa taarifa za mapato na matumizi, hali ambayo itachangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mwezeshaji wa mafunzo ya mifumo mipya kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Nd. Mwita Michael (katikati) akiwaelekeza baadhi ya washiriki namna ya uingizaji taarifa katika mfumo wa DHIS2.
Kwa upande wake DKT. Mtengwa D.M Kwa niaba ya Mganga mkuu wa Wilaya amesema mafunzo hayo yatasaidia kuhakikisha watoa huduma katika vituo vya afya wanapata ujuzi wa kutosha katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mafunzo hayo ya Kielektronikia ni pamoja na DHIS2 (mfumo wa utoaji taarifa za afya), GoTHoMISv3 (mfumo wa utoaji taarifa za ukusanyaji wa mapato ya hospital) na FFARS (mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha) yanayotolewa na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (Public Sector System Strengthening –PS3) kupitia shirika la Maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.