Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Johari Samizi amewataka watoa huduma za maji vijijini wakishirikiana na watendaji wa vijiji na kata kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji.
Ameyasema hayo leo tarehe 14, Disemba 2022 kwenye Mkutano Mkuu wa nusu mwaka wa vyombo vya watoa huduma za maji ngazi ya jamii.
“ naelekeza vyanzo vyote vya maji vitunzwe kwa kupanda miti tena viongozi msiruhusu watu kujenga karibu na vyanzo vya maji wafukuzeni wote awe mganga wa jadi, mzee wa mira na watu wengine kama anavunja sheria achukuliwe hatua” amesema Samizi
Aidha Mkuu huyo amewataka wataalamu wa RUWASA kutatua changamoto zinazopelekea upotevu wa maji kwa asilimia 18 hii imetokana na taarifa waliyoiwasilisha ikionyesha upotevu wa maji asilimia hizo
“ wataalamu tuangalie namna ya kupunguza upotevu wa maji haiwezekani maji yapotee asilia 18 hayo ni maji mengi sana ukizingatia bado kuna maeneo yanachanga.oto za maji, tatueni hilo mkutano ujao hii changamoto isiwepo” Samizi
Naye Meneja wa RUWASA Wilaya Mhandisi Godliver Gwambasa amewataka watoa huduma za maji ngazi ya jamii kuutumia mkutano huo kubadirishana uzoefu na kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii na kukumbushana majukumu
“ lengo la mkutano huu nikukumbushana majukumu, kufanya tathmini ya uendeshaji wa miradi ya maji vijijini, kupata taarifa na takwimu za mapato na matumizi vilevile watoa huduma ya maji wautumie mkutano huu kubadirishana uzoefu katika kutatua changamoto mbalimbali”
Wakiwasilisha taarifa za huduma za màji vijijini watoa huduma za maji ( CBWSO) wamesema pamoja na upatikanaji wa maji bado kuna changamoto ya utunzaji wa miundombinu ya maji hali inayopelekea mabomba kupasuka hivyo kuongeza upotevu wa maji.
Wadau wa maji walioshiriki mkutano huo wameshauri utunzaji wa miundombinu ya maji uzingatiwe na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji wa maji katika misimu yote yaani masika na kiangazi
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.