Uongozi wa Chama cha Watu Wasioona Kwimba “TLB” Umefanya mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 28 November, 2017 hadi tarehe 12 Disemba, 2017. Lengo likiwa ni kuhamasisha walemavu kushiriki katika ngazi za maamuzi na kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo wanayoishi.
Akizungumza katika ziara ya uhamasishaji Mratibu wa Shilika lisilo la kiserikali MNGON (Umoja wa NGOs katika Mkoa wa Mwanza) Ndg Adam Ndokeji alisema walemavu wanatakiwa kushiriki katika mikutano ya Vitongoji, Vijiji, Kata na kutoa maamuzi ili waweze kuainisha mahitaji na changamoto zao.
Mratibu wa Shilika lisilo la kiserikali MNGON (Umoja wa NGOs katika Mkoa wa Mwanza) Ndg Adam Ndokeji akiongea na washiriki wa mkutano katika kata ya Ilula
Aidha Mratibu wa Chama cha Wasioona Kwimba ameiomba jamii kuhakikisha inaboresha miundombinu katika majengo yanayotoa huduma za jamii ili kupunguza changamoto zinazowakabili walemavu.
Naye katibu wa Chama Cha Watu wasioona Kwimba Ngd Salu Kaswahili aliwaagiza walemavu wafanye kazi kwa bidii ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Hata Maandiko Matakatifu ya Mungu yanasema asiyefanya kazi na asile”
Kwa kuongezea Mkuu wa kitengo cha Elimu Maalumu Bibi Elizabeth Tenga aliwaaagiza wazazi kuhakikisha wanawaandikisha watoto wenye ulemavu shuleni kwani wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.
Mkuu wa kitengo cha Elimu Maalumu Bibi Elizabeth Tenga akitoa Mada katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Iseni kijiji cha Nyanshana
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Ilula Bibi Pendo sawe ameiasa jamii inayowanyanyapaa watu wenye ulemavu.
“Tusiwanyanyapae tuwathamini na kuwaheshimu watu wenye ulemavu na tuwape fursa sawa kama watu wengine wasiokuwa na ulemavu”
Aidha Ndg Charles lucas mshiriki kutoka kijiji cha Isegeng’he kata ya Mwakilyambiti alimuommba mwenyekiti wa kijiji kuhakikisha walemavu wanapata nafasi za uongozi sawa na wasio walemavu.
Ndg Charles lucas mshiriki kutoka kijiji cha Isegeng’he kata ya Mwakilyambiti akichangia mada.
Mikutano hiyo ya hadhara ilifanyika katika kata ya Igongwa, Mwagi, Bungulwa, Nkalalo, Iseni, Nyambiti, Ngh’undi, Walla na Ilula Wilayani Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.