Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndug.Nyakia Ally amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuwasisitiza watumishi wote kufanya kazi na kila mtu kutimiza wajibu wake, haya yamejitokeza leo tarehe 02/02/2021 kwenye baraza la wafanyakazi ambapo Katibu Tawala alikuwa mgeni rasmi akimuwakirisha Mkuu wa Wilaya.
Katika kikao hicho Katibu Tawala amewataka watumishi wote kufanya kazi kwa bidii na kuepuka migogoro kazini,vilevile amewataka watumishi wote kuwa tayari kuonyana na kuwa tayari kuonywa pale mtu anapokuwa nje ya utaratibu na amesisitiza maonyo yafanyike kwenye vikao vya kawaida vya kisheria
Aidha amewataka watumishi kuwa waadilifu hasa wale wanaojihusisha na majukumu mengine wayafanye baada ya muda wa kazi, pia amemtaka Afisa utumishi kufuatilia watumishi wasiofanya kazi masaa yote ya kazi ili wachukuliwe hatua.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri Bib.Pendo Malabeja amesisitiza watumishi wote kupendana,kuheshimiana na kufanye kazi kwa mujibu wa sheria za ajira , pia amewataka viongozi wa vyama vya wafanyakazi waliohudhuria kikao kuwa mabalozi kwa watumishi wengine.
Bib Pendo Anangisye Malabeja Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba
Muwezeshaji wa kikao hiki Ndug.Goodluck Luginga Afisa Kazi kutoka kwa kamishina wa Kazi amesema Baraza la watumishi ni kilainishi kati ya mwajiri na watumishi hivyo baraza hili linapaswa kutumika kama chachu ya maendeleo kwa Halmashauri na watumishi wote.
Goodluck Luginga Afisa Kazi kutoka kwa Kamishina wa Kazi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.