Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wameaswa kufanya kazi kwa bidii,uwajibikaji na uadilifu, haya yamejitokeza katika kikao kazi kilichofanyika tarehe 15/04/2021 Shule ya Sekondari Nyamilama..
Akiongea katika mafunzo hayo Afisa utumishi Ndug.Israel Petro amewataka watumishi wote wa umma kufanya kazi kulingana na kanuni na utaratibu wa utumishi wa umma.Aidha amewataka watumishi wote kujaza OPRAS( fomu maalumu ya kupima mikakati na uwajibikaji wa watumishi) ili kuonyesha mikakati na malengo yao ya utendaji kazi kwa mwaka mzima na amewataka kuhakikisha wanatimiza malengo wanayojiwekea.
Naye Bi.Angera Mulisa Afisa utumishi amewaasa watumishi wote kuwa waadilifu,wawajibikaji,nidhamu na uaminifu katika kazi,amewashauri wahudumu wa Afya kutoa huduma kwa weredi bila ubaguzi na kuwa na kauli nzuri kwa wagonjwa.Bi Angera amesisitiza kuwa watumishi wa Umma wanapaswa kuwa watu wa mfano mzuri katika jamii hivyo muonekano wao,tabia zao na matendo yao vyote vinapaswa kuendana na utumishi wa Umma.
Katika mafunzo hayo Ndugu Nyanda Shimiyu amewaelekeza watumishi wote jinsi ya kupata haki zao za Msingi kama likizo na ruhusa na amewashauri kuwa makini wanapojaza fomu mbalimbali zinazohusiana na kazi zao.
Aidha Mwalimu Richard Hangaya Katibu wa Tume ya Waalimu(W) (TSS) amewataka Walimu na Watumishi wengine kuwa wazalendo,watii kwa viongozi wa kazi zao,watii kwa Taifa na amewataka kutoa huduma bora, kila mtu katika nafasi yake ya kazi atimize wajibu wake.
Maafisa hao wamefanya mafunzo hayo kwa watumishi wote wa Wilaya ya Kwimba kwa lengo la kukumbushana wajibu wa kila mtumishi katika eneo lake la kazi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.