Wazazi wa wanafunzi ambao hawajaripoti kidato cha kwanza mpaka leo tarehe 4 March, 2022 watakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na jeshi la police.
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi leo March 4 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Akiogea katika Mkutano huo Mheshimiwa Samizi amesema
" Hatutawaonea haya wazazi wote ambao kwa utashi wao wameona ni vyema watoto wao wasisome,tutawakamata na kuwachukulia hatua kali"
Mkuu huyo amesema kuwa wanafunzi zaidi ya 1000 bado hawajaripoti kidato cha kwanza hivyo kuanzia tarehe 7 March itafanyika operesheni kubwa ya kuwakamataza wazazi wa wanafunzi hao.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Madiwani kushiriki katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi inayoendelea katika maeneo yao ya utawala.Amesisitiza kuwa Wilaya ya Kwimba imeshapokea zaidi bilioni 16 kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Halmashauri na Taasisi nyingine ikiwemo Wakala wa maji vijijini( RUWASA), VETA,Chuo cha Afya ,Chuo cha michezo na Taasisi nyingine.
Katika baraza hilo Waheshimiwa Madiwani wameunga mkono hoja ya kufatilia wanafunzi kuripoti Shuleni na wameahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanafunzi wote wanapata Elimu.
Akisoma taarifa ya Halmashauri Bi. Happiness Msanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amesema Halmashauri imeshapokea 76% ya bajeti yote ya mwaka wa fedha, hivyo iko miradi mingi inayotekelezwa ikiwemo ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati, madarasa, Shule mpya mbili, Nyumba za Waganga,nyumba ya Mkurugenzi,Ujenzi wa Jengo la Halmashauri na miradi mingine.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.