Mkurugenzi wa Sera na mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI Ndugu. John Mihayo Cheyo amewaasa wazazi wa wanafunzi kuhakikisha wanaimarisha usalama wa wanafunzi, huku wakihakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayeacha masomo kwa sabanu ya utoro,mimba, kuoa au kuolewa na mambo mengine.
Ameyasema hayo jana Oktoba 7,2023 kwenye mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari Bupamwa ambapo alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hiyo
"wazazi saidieni watoto wasiache Shule, pendeni kuona mafanikio ya watoto wenu wakimaliza Shule na kufaulu,zuieni utoro, narudia tena wanafunzi wasilale nyumbani wakawa watoro shuleni na wasiolewe " amesema Cheyo
Shule hiyo imeonekana kuwa na changamoto ya utoro na baadhi ya wanafunzi kuacha Shule kwani wanafunzi waliohitimu ni 93 kati ya 153, wengi wameonekana kuacha Shule kwa sababu ya umbali kutoka nyumbani kwao hadi shuleni na sababu nyingine
" tumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ameiona changamoto waliyokuwa wanaipata wanafunzi wanaotokea vijiji vya Itegamatu, Kiliwi na Dodoma sasa ameleta fedha, Shule mpya inajengwa Kiliwi nadhani hatutasikia tena wanafunzi watoro au kuacha Shule" Cheyo
Katika mahafali hiyo mgeni rasmi ametatua changamoto za Shule hiyo ikiwa ni pamoja na kununua tangi la maji la thamani ya milioni 1.5 ili kuhakikisha upatikanaji wa Maji shuleni, vilevile changamoto nyingine zikiwemo za miundombinu ya mabweni ameahidi kwenda kufuatilia wizarani Ili miundombinu hiyo ikamilishwe.
Mkurugenzi huyo amewahamasisha Walimu na watumishi wengine wa Shule hiyo kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza ufaulu wa Shule hiyo "leo nimekuja na zawadi za wanafunzi waliofanya vizuri, Walimu na wapishi, niwaombe muendelee kufundisha vizuri na kuwasaidia wanafunzi wote wafaulu,nawapongeza sana kwa kufuta ziro matokea ya kidato cha nne mwaka jana muendelee hivyo msirudi nyuma" Cheyo
Mkuu wa Shule hiyo Mwl.Herman Shingisha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya kiongozi shupavu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za ujenzi wa madarasa na hivyo kuondoa kero ya uhaba wa madarasa na Shule mpya.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.