Mhe:Luhaga Joseph Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi atembelea wilaya ya Kwimba kata ya Maligisu na kuongea na wananchi wa kata hiyo.Akiongea na wananchi amewaeleza jinsi wizara ilivyopunguza bei za dawa kwaajili ya mifugo na hivyo kurahisisha gharama za ufugaji bora amesema "tumepunguza gharama ya uogeshaji mifugo kutoka shilingi 12,000 kwa mwaka hadi 1200 kwa ng'ombe".Aidha amewataka wananchi kuanzisha ufugaji wa samaki ili kujiongezea kipato na kitoweo kwa ajili ya familia na ameahidi kutoa vifaranga vya samaki bure kwa Halmashauri itakayoanzisha mradi huo mapema.Waziri ameahidi kukarabati majosho yasiyopungua matatu na akaitaka Halmashauri kukarabati majosho yatakayokua yamebaki.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.