Waziri wa Utamaduni,Sanaa na michezo Mhe. Dkt Damas Ndumbaro amewataka wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha michezo na ujenzi wa hosteli vinavyojengwa chuo cha michezo Malya kuhakikisha majengo yanakuwa na ubora unaotakiwa.
Ameyasema hayo Leo Julai 1,2024 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo " nikiangalià ubora wa haya matofari unatia shaka, tofali zinaanza kubomoka hakikisheni ubora unazingatiwa kumbukeni Mheshimiwa Rais ameweka fedha Bilioni 32 siyo kitu kidogo" amesema Ndumbaro
Waziri huyo amesisitiza kuwa ubora wa majengo ndio utawavutia wacheza na wadau wengine kuja kutumia viwanja vya michezo vinavyojengwa chuoni hapo
"kwenye hiyo maktaba lazima kuweka eneo watakalo kaa wakufunzi wakutoka nje ya nchi ili tukimtoa mkufunzi Ujelumani aje akae vizuri afundishe" amesema Ndumbaro
Aidha Mheshimiwa Ndumbaro amesisitiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo kusimamiwa ili atekeleze kwa ubora na kwa wakati " hatuna shaka na mkandarasi huyu lakini asimamiwe ili mradi ukamilike kwa wakati na kwa ubora"
Naye Mkuu wa chuo hicho amesema mradi huo unatarajia kutumia bilioni 32 mpaka kukamilika awake, ambapo ujenzi wa viwanja,madarasa, hostel, na kantini yameanza kujengwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.