Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Ng'wilabuzu Ludigija Leo Aprili 24,2023 amezindua wiki ya chanjo Kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, chanjo zilizotolewani pamoja na chanjo ya kuzuia kupooza, kukinga surua, kukinga kuhara na magonjwa mengine.
Uzinduzi huo umefanyika katika Kijiji cha Shirima Kata ya Kikubiji ambapo wazazi wenye watoto wamefika na kupata chanjo hizo, watoto hao wamepewa chanjo kulingana na umri wa mtoto na kuzingatia aina ya chanjo ambazo mtoto alishapewa.
Watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 wamepewa chanjo ya kukinga saratani ya shingo ya kizazi.Pia wazazi wamesisitizwa kuitumia wiki hii kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo za magonjwa mbalimbali Ili waweze kuwakinga watoto wao
"tuko kwenye maadhimisho ya wiki ya chanjo na sisi Kwimba tumeamua wiki hii tuiadhimishie Kikubiji lengo ni kuhakikisha Wananchi wa kata hii wanapata huduma hii maana viongozi wenu waliomba tulete chanjo huku kwenu, niwapongeze wanafunzi wakike waliokuja kupata chanjo ya saratani, ugonjwa wa saratani ni hatari sana kwahiyo lengo la chanjo hii nikuwakinga watoto wetu na magonjwa yanayoweza kuzuilika" Ludigija
Mkuu huyo amesisitiza kuwa chanjo hizo ni salama hivyo Wananchi wasione shaka kuwaleta watoto kupata chanjo
Katika uzinduzi huo ameshiriki Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Thereza Lusanga ambaye amewahimiza wanawake wajawazito kuhakikisha wanajifungua katika vituo vya Afya
"nawapongeza Sana kwa mwitikio wenu wa kuwaleta watoto kupata chanjo pia niwashauri wanawake wajawazito msijifungulie nyumbani hakikisheni mnafika kwenye huduma za Afya Ili muokoe maisha yenu na watoto"
Aidha Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Shija Malando ameitumia nafasi hiyo kuwaeleza Wananchi miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Kata hiyo "kazi yetu Chama ni kufuatilia na kuikumbusha Serikali kwa mfano hapa Kikubiji mmepata fedha za ujenzi wa kituo cha Afya millioni 500, mmejenga madarasa, barabara zimeboreshwa haya yote ni matokeo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" Malando
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi wote waliowaleta watoto kupata chanjo hizo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.