Akiongea katika kikao cha makabidhiano ya mradi wa boresha kilichofanyika leo tarehe 20 Agosti,2021 kwenye Ukumbi wa Ndilima Hungumalwa, Mkurugenzi wa mradi huo Bi.Saida Salum Mukhi amesema katika Mkoa wa Mwanza ni Wilaya ya Kwimba pekee ambayo wanaume zaidi ya elfu nne wamejitokeza kupima virusi vya UKIMWI choni ya mradi wa boresha ukilinganisha na Wilaya nyingine.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo wakati akitoa maelezo mafupi ya namna mradi wa boresha ulivyofanyakazi, kabla ya kukabidhi mradi kwa muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mganga wa Wilaya Daktari Elias Misana. Aidha katika tukio hilo muwasilishaji wa taarifa ya mradi Ndug. Respectson Akyoo amesema jumla ya wanaume 4535 wamepima UKIMWI ambapo 590 kati ya hao wamekutwa wameàthirika na wanawake 3355 wamepimwa 497 kati yao wameathirika. Aidha Akyoo ameuomba uongozi wa Wilaya kuuendeleza mradi pale walipoishia ili uhamasishaji kwa wanaume kuhusu kupima UKIMWI uendelee,hamasa kuhusu kuzuia ukatili wa kijisinsia na michezo kwa watoto iendelezwe.
Mradi wa boresha ulikuwa ukifadhiliwa na Shirika la TIP( Tanzania Interfaith Partnership) ambapo mradi huu ulijishughulisha na kutoa elimu juu ya kuzuia ukatili wa kijinsia, kuhamasisha wanaume kupima virus vya UKIMWI, na michezo kwa vijana wa kiume ambao kupitia michezo hiyo walifundishwa kuwa mabalozi wa kuzuia ukatili kwa watoto wa kike.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.