Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amezindua huduma za Afya katika Zahanati ya Sangu katika Kijiji cha Sangu Kata ya Mhande.Uzinduzi huo umefanyika Leo April 24,2023
Akizindua Zahanati hiyo Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya Zahanati hiyo Ili iweze kufanya kazi na kudumu Kwa muda mrefu,pia amewashauri Wananchi hasa wanawake wajawazito kuhakikisha wanatumia Zahanati kupata kuhuma za kiafya
"niwasihi Wananchi inawezekana mmesubiri kwa muda mrefu kupata Zahanati hii sasa mmepata itumieni vizuri,wataalam wa Afya wapo, niwaombe mtoe ushirikiano Kwa wataalam waafya na Sasa wanawake hatutarajii kusikia wanajifugulia nyumbani, maana huduma imesogezwa karibu vilevile acheni kutumia dawa za mitishamba mkiwa wajawazito maana ni hatari Kwa mtoto aliyeko tumboni" Ludigija
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi kuendelea kujikinga na malaria Kwa kuhakikisha wanalala kwenye chandarua " tumegawa vyandarua 12,0000 Ili kuhakikisha tunawakinga hasa watoto na ugonjwa wa malaria, ugonjwa huu ni hatari sana umeendelea kusababisha Vifo kwahiyo tunahimiza wananchi mtumie vyandarua Ili kujikinga, lengo la Serikali ni kuhakikisha angalau asilimia 80 ya Wananchi wanalala kwenye chandarua"
Mkuu huyo amekemea tabia ya baadhi ya Wananchi wanaotumia mavuno yao vibaya na hivyo kusababisha njaa kwenye familia, amewataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja na watakaobainika watachukuliwa hatua " usiumize familia yako kwa kuchukua mazao na kwenda kunywea pombe au kufanya mambo ambayo hayana faida Kwa familia"
Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Happiness Msanga amewapongeza wananchi kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo ambalo Wananchi walianzisha na Serikali ikakamilisha, vilevile amewahakikishia Wananchi kuwa huduma zitakazotolewa katika Zahanati hiyo zitakuwa bora kwasababu kuna wataalamu watatu ambao wameshapangiwa kufanya kazi hapo.
Nao Wananchi wameishukuru Serikali kwa kukamilisha Zahanati hiyo " tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru Mkuu wa Wilaya na viongozi wote kutukamilishia Zahanati yetu tulisubiri Kwa muda mrefu Sana hatimaye leo tunaanza kupata huduma hapa karibu" Anton
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.