Akiwasilisha taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amesema zaidi ya bilioni 20 zimepokelewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.Taarifa hiyo imewasilishwa leo tarehe 29 Machi, 2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Michezo Malya.
Miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa Shule mpya mbili, ujenzi wa madarasa na ukamilishaji wa madarasa na maabara. Miradi mingine ni ujenzi wa Vituo vya afya vinne, ukamilishaji wa Zahanati nne, ununuzi wa vifaa tiva na ujenzi wa Jengo la dharura na jengo la upaasuaji katika hospitali ya Wilaya.
Mheshimiwa Samizi amisisitiza kuwa Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa kwani ameleta fedha nyingi kwenye Taasisi mbalimbali ikiwemo TARURA ambapo miradi ya barabara na madaraja inaendelea kutekelezwa huku RUWASA wakiendelea kuongeza mtandao wa maji na ujenzi wa matangi maeneo mbalimbali,nao Tanesco wameendelea kusambaza Umeme vijijini, Chuo cha Afya Ngudu kikikarabatiwa ,Ujenzi wa Chuo cha VETA ukielekea kukamilika na Chuo cha Michezo Malya ujenzi wa Hostel na jengo la michezo ukiendelea kutekelezwa.
" miradi inayotekelezwa ni mingi sana kwahiyo hatunabudi kumshukuru Mama Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu anaupiga mwingi Kwimba" amesema Samizi
Katika Hafla hiyo Wananchi wamemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali na kuwaongezea miundombinu ya Elimu, Afya na maji
"ninamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwakutuletea fedha za miradi hasa ile ya elimu, Afya na maji maana kunamaeneo mengine maji yalikuwa hayajafika lakini sasahivi watu wengi wanatumia maji ya ziwa tunashukuru sana" amesema Milembe Nyanda
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.