Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepokea bilioni 4.9 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo,ikiwa ni pamoja na miradi ya Elimu na Afya.
Akiwasilisha taarifa ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23 kwenye baraza la Madiwani, lililofanyika leo tarehe 9, Novemba 2022 kwenye ukumbi wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema
“ Halmashauri imepokea bilioni 4.9 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo bilioni 2.24 ni za ujenzi wa madarasa 112 katika Shule za Sekondari, bilioni 2.5 ni fedha za ujenzi wa nyumba za waganga na ununuzi wa vifaa tiba vya Hospitali ya Wilaya na Vituo vya Afya vinne pamoja na ukamilishaji wa zahanati”
Katika baraza hilo weheshimiwa Madiwani wameelekezwa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao ili kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri
“ Madiwani kasimamieni mapato, hayo mapato ndiyo yanayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mapato ya ndani, diwani hujishirikishi kukusanya mapato lakini unataka posho iongezwe, unataka utekeleze miradi kwenye kata yako haya yote hayawezi kufanyika bila kukusanya mapato” amesema DC Samizi
Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuimarisha ulinzi na usalama kwa Wananchi, amesema hilo kufatia tukio lililotokea wiki iliyopita la mauaji ya Albino katika kijiji cha Ngula
“ inasikitisha sana kuona mtu ameuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wakaondoka na mkono hii hali ni mbaya sana, nawaelekeza Madiwani mkaboreshe ulinzi,shirikianeni na jeshi la Sungusungu kuimarisha ulinzi, hakikisheni kila mtu anakuwa mlinzi wa mwenzake” amesema Samizi
Madiwani walioshiriki baraza hilo wameahidi kwenda kufanya kazi zao ikiwa ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo
“ Mimi ni miongoni mwa madiwani walionufaika maana katika kata yangu tumeookea milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa Shule ya msingi mpya ya Mwaluleho" àmesema Stephano Cheyo Diwani Kata ya Bupamwa
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.