Wananchi wa Kijiji cha Mwang'ombe Kata ya Hungumalwa wanatarajia kunufaika na huduma za Afya zilizoanza kupatikana Leo November 11,2023 baada ya Zahanati hiyo kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija.
Akifungua Zahanati hiyo Mheshimiwa Ludigija amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha milioni 50 kwaajili ya kukamilisha jengo hilo la Zahanati.
Aidha Ludigija amewapongeza Wananchi wa Kijiji kwa kuanzisha ujenzi wa Zahanati hiyo Kwa nguvu zao pia amewashauri kuitunza miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwahudumia kama ilivyokusudiwa.
Mkuu huyo amewasisitiza wananchi wote hasa wanawake wajawazito kuitumia zahanati hiyo kupata kuduma za kliniki na kujifungua " wanawake wajawazito hakikisheni mnahudhuria kliniki na kujifungua hapa Zahanati ili kujiepusha na vifo vinavyotokea kwa wale wanaojifungulia nyumbani" Ludigija
Akiwasilisha taarifa fupi ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema Zahanati hiyo imejengwa kwa milioni 60.3 ambapo Wananchi walijenga boma Kwa milioni Saba,Mbunge wa Jimbo la Kwimba na wadau na Halmashauri nao walichangia huku Serikali kuu ikitoa milioni 50 kwaajili ya ukamilishaji.
Wananchi wa Kijiji hicho wamemshukuru Rais kwa kuwajengea Zahanati hiyo " tunamshukuru Rais kwa kutujengea hii Zahanati, tulikuwa tunatembea umbali mrefu kupata huduma za Afya sasa tutahudumiwa hapa karibu" Leokadia John
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.